Kabla ya kuzuka kwa Covid-19, kundi la B2C kutoka uganda lilifanikiwa kuandaa matamasha mawili lakini kwa bahati mbaya walilazimka kusitisha kutokana na makali ya corona.
Baada ya kufunguliwa tena kwa uchumi nchini uganda, B2C wiliahidi kuandaa maonyesho mapya.
Sasa habari njema ni kwamba wasanii wa b2c wametangaza tarehe ya tamasha lao lijalo.
Kupitia mitandao yao ya kijamii, tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe Septemba, 16 mwaka wa 2022.
Sehemu ambayo tamasha hilo litafanyika bado haijathibitishwa lakini duru za kuaminika zinasema kuwa tamasha la B2C litafanyika Freedom City.
Wasanii wengine wanaotarajiwa kufanya matamasha yao ya muziki mwaka huu ni pamoja na Jose Chameleone, na Pallaso.