You are currently viewing BAADHI YA WADAU WA MUZIKI WATAKA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA KUAHIRISHWA

BAADHI YA WADAU WA MUZIKI WATAKA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA KUAHIRISHWA

Katibu mkuu katika chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA Phina Mugerwa hajafurahishwa na namna ambavyo uchaguzi wa chama hicho utafanyika juni 28 mwaka huu huko National Theatre Kampala.

Tume ya uchaguzi katika chama cha uma iliahirisha uchaguzi wiki kadhaa zilizopita baada ya visa vya udanganyifu kuripotiwa.

Tume hiyo ikaamua kufanya uchaguzi kwa njia ya kawaida ya kupiga foleni kwenye vituo vya kupigia kura katika kituo kimoja jijini kampala.

Lakini  kwa Phina Mugerwa ambaye anawania wadhfa wa ukatibu mkuu kwa mara ya pili katika chama cha uma amesema kuwa sio jambo la kingwana kutowajumuisha wapiga kura kutoka mashinani kwenye uchaguzi huo ikitokea wameshindwa kusafiri hadi kampala kwa ajili ya kushiriki uchaguzi.

Phina Mugerwa amedai kuwa maeneo mengine ya nchi ya Uganda inaundwa na asilimia 70 ya chama cha UMA na mfumo wa kituo kimoja cha kupigia kura utawanyima wasanii wengine uhuru na haki yao ya kupiga kura kama katiba inavyoainisha.

Hata hivyo ametaka tume ya uchaguzi katika chama cha UMA kuahirisha uchaguzi wa chama hicho hadi pale mfumo utakaowajumuisha wapiga wote utakapobuniwa.

Utakumbuka King Saha kupitia mawakili wake Lukwago & Co. Advocates walitoa lalama zao kwa tume uchaguzi ya chama cha uma kuhusu mfumo wa upigaji kura kwa njia ya mtandao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke