You are currently viewing BABA MZAZI WA PETER MIRACLE BABY ALIA KUPITIA MAISHA MAGUMU, AOMBA MSAADA WA KIFEDHA

BABA MZAZI WA PETER MIRACLE BABY ALIA KUPITIA MAISHA MAGUMU, AOMBA MSAADA WA KIFEDHA

Wakati msanii Peter Miracle Baby anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Mugithi, kumbe Baba yake mzazi hana makazi na anapitia maisha magumu sana mtaani.

Kupitia video ambayo inasambaa mtandaoni Mzee David Ndolo maarufu Notorious, ameonekana mtaani akiomba msaada kwa kijana wake huyo ambaye hawana mahusiano mazuri.

Mzee huyo amesema kuwa hafurahishwi kabisa na maisha anayoishi mtaani ambapo amemtaka Miracle Baby kuingilia kati na kumtoa kwenye maisha ya uchochole.

“Niaje wathii, mi ndio baba Miracle Baby, anaitangwa Willy Mpole, nimemzalia hapa Mlango Mkubwa…Anaitangwa Miracle Baby Wilson … Mimi naitangwa David Ndolo … Mi ndio baba yake nimemzaa … siezi kubali hiyo maisha ju ni ya shida nay a kuteseka na kusononeka Zaidi,” alisema.

Miracle Baby hata hivyo amejibu tuhuma hizo kwa kejeli kwa kuandika “Niseme Nini mimi willy mpole na msee mwingine asiniulize kuhusu babangu tena kwani coz sikujizaa mm na amjuae baba ya mtoto ni mama so io swali si yangu kujibu “

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke