Meneja wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi kwa ujumla, Babu Tale amesema sio kweli kwamba Sallam SK anajiunga na Lebo ya Harmonize, Konde ‘Gang’ Music Worldwide.
Tale amesema amefurahi kuona wawili hao wamemaliza tofauti zao kama ilivyoonekana mitandaoni hivi karibuni lakini sio kweli suala kujiunga na Lebo yake.
“Lakini nilipoona juzi wanasalimiana maana yake hakuna shida, ila hii ya kusema Sallam SK kakumbatiana na Harmonize anaenda Konde Gang, eeh, we kuweza!” amesema Babu Tale akiongea na Mjini FM.
Itakumbukwa, Sallam anahusishwa zaidi kuwa ndiye atakaye kuwa Meneja wa Harmonize kufuatia video inayowaonesha wawili hao wakisalimiana na kukumbatiana walipokuwa visiwani Zanzibar ambapo Sallam alihudhuria kwenye show ya Harmonize jambo ambalo limeibua hisia chanya kwa mashabiki.
Sallam SK ni miongoni mwa Mameneja wa watatu wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi, wengine ni Babu Tale na Mkubwa Fella.