Aliyekuwa mke wa Mejja, Milly Wairimu amejipata pabaya kwenye mitandao ya kijamii baada ya walimwengu kumshambulia kwa madai ya kumvunjia heshima msanii huyo kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake Mei, 23.
Kwenye ujumbe wake aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii Milly Wairimu alimtakia Mejja heri ya siku ya kuzaliwa na kusindikiza na matusi yakimtakia msanii huyo maisha mabaya kutokana na maovu aliyomtendea kipindi wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Sasa ujumbe huo umeonekana kuwakera mashabiki wa Mejja ambao wameshushia kila aina matusi mrembo huyo huku wakimtaka akubali kwamba mahusiano yake na Mejja yalivunja kitambo na badala yake atafute mpenzi wa ndoto yake atakayemliwaza.
Utakumbuka mwaka 2021 Milly Wairumu alijitokeza hadharani na kutangaza mtandaoni kwamba waliachana na mejja baada ya msanii huyo kumsaliti kimapenzi.