Baby Mama wa msanii Mikie Wine, Shazney Khan, amewapa somo wanawake kipindi hiki ambacho kumekuwa na tetesi kuwa mahusiano yake yameingiliwa na jini mkata kamba.
Khan ambaye alimtambulisha Wine kwa wazazi wake mwezi Oktoba mwaka 2021, mewashauri wanawake kutowachumbia wanaume ambao wanajihusisha na masuala ya Sanaa nchini Uganda.
Mwanamama huyo mwenye makasiriko, amesema wasanii wengi ni wasaliti kwenye mahusiano kutokana na hulka yao kuwaumiza wanawake kimapenzi.
“Ushauri… Usimchumbie mwanaume katika tasnia ya muziki nchini Uganda. Watakuvunja moyo bure,” aliandika kwenye WhatsApp story yake.
Kauli ya Shan imekuja siku moja baada ya kufuta picha zote alizopiga na Wine ambaye wamezaa watoto wawili kwa pamoja kwenye mtandao wa Instagram.
Kwa sasa Wine anafanya vizuri na wimbo uitwao “Mwali Bana” aliyomshirikisha Chosen Becky, wimbo ambao ulitayarishwa na prodyuza Paddy Man.
Wawili hao wamekuwa wakiposti misusuru ya video kwenye mtandao yao ya kijamii wakiwa kwenye mahaba mazito kwa lengo la kutangaza kazi yao mpya.