Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Sonnie, ametangaza kupiga mnada na kuuza dread locks zake ambazo alinyoa juzi kati.
Kwenye kikao cha maswali na majibu katika mtandao wa Instagram na mashabiki zake, Mrembo huyo amesema anauza nywele hizo kwa shilling laki 3 za Kenya na yeyote anayehitaji amtafute kwenye mitandao ya kijamii ili waweze kufanikisha mchakato wa manunuzi.
Hata hivyo hatua hiyo imeonekana kuzua mjadala mzito miongioni mwa watumiaji wa mitandao wengi wakihoji huenda mrembo huyo atafuta mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni ikizingatiwa kuwa hakuna atakayenunua dread locks hizo hapa nchini.
Kumbuka dread locks hizo ni za mwaka wa 2013 na Carol Sonnie amekuwa akizifanyia maboresho mara kwa mara licha ya watu kumshinikiza kuzinyoa.