Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Muthoni amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu ya kutoka kimapenzi na msanii Madini Classic.
Kupitia Instagram page yake Carol Muthoni amepuzilia mbali suala la kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo huku akionesha kushangazwa na kitendo cha Madini Classic kutumia jina lake kutafuta kiki ya kutangaza ujio wa wimbo wake mpya.
Mrembo huyo amewataka mashabiki zake kutoamini madai yanaosambaa mtandaoni kuwa anatoka kimapenzi na Madini Classic kwa kusema kuwa walikuwa wanatayarisha video ya wimbo mpya ya msanii huyo.
Kauli ya Carol Muthoni imekuja mara baada ya Madini Classic kushare picha ya pamoja na mrembo wakiwa kwenye pozi la kimahaba zaidi ambapo alienda mbali zaidi na kuthibitisha kuwa mrembo huyo amekubali kuwa mke wake wa pili