You are currently viewing Bahati adai wakosoaji wake mtandaoni wanampa nguvu ya kutia bidii kimuziki

Bahati adai wakosoaji wake mtandaoni wanampa nguvu ya kutia bidii kimuziki

Mwanamuziki kutoka Kenya Bahati amedai kwamba hana muda wa kuwajibu wanaomkosoa mtandaoni.

Hitmaker huyo wa Adhiambo amewaambia watesi wake kuwa chuki anayoipata kwenye mitandao ya kijamii inampa changamoto ya kutia bidii kwenye kazi zake za muziki.

“Guys thank you so much for your support. Like we wouldn’t be here without you without your love, without your criticism, negativity, we take them in”, Aliandika Instagram.

Bahati alisema hayo alipokuwa akizindua tuzo ya Golden Plaque aliyotunukiwa na mtandao wa YouTube kwa ajili ya kupata wafutialiaji (Subscribers) milioni moja.

Bahati na mke wake Diana B wamekuwa wakikosolewa mitandaoni mwaka mzima kwa matukio ambayo wamekuwa wakijihusisha nayo na hawajaathirika kwa namna yeyote kwenye shughuli zao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke