Wakati bado Bahati anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nowe Sweety,’ ameonyesha kuwa hataki kulaza damu kuhusu muziki,ameonekana ujio wa kazi yake mpya na msanii wa BongoFleva Harmonize.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bahati amepost picha akiwa na Harmonize na kuandika ‘2023 are You Ready for Us??? Brother @Harmonize_tz ‘ na Harmonize akajibu kwa kuandika ‘SEND IT BRO I HAVE ONLY ONE WATSP NUMBER LOVE YOU NO MARA WAA !!! GETO BOYS ‘.
Iwapo Bahati atafanikiwa kuachia wimbo wake na Harmonize atakuwa ameongeza orodha ya wasanii wa Bongoflava aliofanya nao kazi ikizingatiwa kuwa ana kazi ya pamoja na Rayvanny, Mbosso na Aslay.