Nyota wa muziki nchini Bahati amefikisha idadi ya subscribers Milioni 1 kwenye mtandao wa Youtube.
Bahati ambaye alijiunga na mtandao wa youtube Agosti 7, mwaka 2012 amepata subscribers wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.
Baadhi ya matukio anayoyaweka katika channel yake ni shoo anazozifanya, video zake za muziki pamoja na utayarishaji wa video za nyimbo zake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” hadi sasa Kupitia channel yake ya YouTube kazi zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni 172 tangu ilipofunguliwa rasmi channel yake ya youtube miaka 10 iliyopita.
Bahati anakuwa msanii wa pili nchini mwenye wafuasi wengi katika mtandao wa youtube baada ya Oitle Brown ambaye ndiye alikuwa msanii wa kwanza nchini kufikisha subscribers milllioni moja youtube.