You are currently viewing BAHATI AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE

BAHATI AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE

Hatimaye staa wa muziki nchini Bahati ameamua kuvunja kimya chake kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza ubunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Kwenye mahojiano na Nairobi News mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amefichua kuwa hali sio shwari katika familia yake hasa upande mke wake Diana.

Bahati hata hivyo amepata kigugumzi kueleza kwa kina kinachoendelea ndani ya familia yake licha mtandao huo kumsisitizia kuweka wazi kinachomsibu.

Siku chache zilizopita Diana aliposti picha ya njiwa mweupe kwenye background nyeusi na kusindikiza na ujumbe unaosomeka ” Only in the Darkness, Can you see the Stars .”

Ujumbe huo uliowaacha mashabiki njia panda ikizingatiwa kuwa alikuwa amezima uwanja wa kutoa maoni kwenye posti yake instagram.

Mashabiki hata hivyo walienda mbali na kuhoji kuwa huenda kuna habari mbaya imemtokea mwanamama huyo ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi nane.

Mara ya mwisho Diana kuonekana hadharini ilikuwa kwenye hafla ya baby shower yake ambapo alifunguka kupitia changamoto nyingi kwenye safari yake ya uja uzito.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke