You are currently viewing BAHATI AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUSHINDWA KULIPA DENI LA SHILLINGI 150,000 ZA KENYA

BAHATI AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUSHINDWA KULIPA DENI LA SHILLINGI 150,000 ZA KENYA

Mwanamuziki aliyegeukia siasa nchini Kenya Bahati amefunguliwa mashtaka na kampuni ya ya mawakili ya Katunga Mbuvi & Co Advocates kwa madai ya kushindwa kumlipa mpiga picha mmoja shillingi 150000 baada ya kumfanyia kazi.

Kupitia barua rasmi waliyomuandikia Bahati tarehe 30 mwezi machi mwaka huu,  kampuni hiyo imemtaka msanii huyo kumlipa mteja wao aitwaye Jeremiah Mathambu Thomas JT Shillingi 150,000 katika kipindi cha siku saba zijazo la sivyo watamfungulia kesi katika mahakama kuu ya nairobi.

Barua hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambao wameonekana kupuzilia mbali tuhuma hizo wakisema kuwa ni njema ya kumchafulia jina Bahati ikizingatiwa kuwa Bahati ni msanii mkubwa ambaye tayari ana timu yake ya kupiga picha na kuchukua video hivyo hawezi mkodisha mtu wa nje.

Hata hivyo mpaka sasa Bahati hajatoa tamko lolote kuhusu kashfa zilizoibuliwa na kampuni ya ya mawakili ya Katunga Mbuvi & Co Advocates dhidi yake ila ni jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke