Mwanamuziki aliyegeukia siasa Bahati ameshindwa kuficha furaha yake baada ya tume ya IEBC kumuidhinisha kuwa atawania ubunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia Tiketi ya chama cha Jubilee.
Kupitia ukurasa wake wa instagram bahati ameandika waraka mrefu wa kuwashukuru kumshukuru mungu, chama cha jubilee na watu wa mathare kwa kumpa nafasi ya kuwawakilisha kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti huku akitoa wito kwa wafuasi wake wampe kura ili aweze kuleta mabadiliko.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema ndoto yake na watu wa mathare imetimia kwa kuwa wamekuwa wakiomba kwa muda kumpata mbunge ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo.
Wasanii wengine walioidhinishwa na IEBC ni mchekeshaji Jalang’o ambaye ni mgombea wa ubunge Lang’at kupitia cha cha ODM, na Mc Jessy ambaye ni mgombea wa ubunge Imenti Kusini.