Staa wa muziki nchini Bahati ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kukabidhiwa tena cheti chake cha kuwania ubunge mathare kupitia chama cha Jubilee
Katika mkao na wanahabari bahati amemshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa nafasi tena kuwania ubunge kwa tiketi ya chama cha Jubilee na kinara wa ODM Raila Odinga kwa kumuamini kugombea ubunge wa mathare kupitia mwavuli wa Azimio la Umoja.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema ndoto yake na watu wa Mathare imetimia kwa kuwa wamekuwa wakiomba kwa muda kumpata mbunge ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo.
Hata hivyo amewashukuru wajumbe wa Jubilee na wakaazi wa Mathare kwa ujumla kwa kumkingia kifua alipony’ang’anywa cheti cha jubilee wiki kadhaa zilizopita huku akitoa rai waendelee kumuunga mkono kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa Mathare.
Kwa sasa Bahati anatarajiwa kumenyana na wapinzani wake kutoka vyama mbali mbali kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.