You are currently viewing BAHATI AKANUSHA MADAI YA KUTUMIA UBUNIFU WA EDDIE BUTITA BILA RIDHAA YAKE

BAHATI AKANUSHA MADAI YA KUTUMIA UBUNIFU WA EDDIE BUTITA BILA RIDHAA YAKE

Staa wa muziki nchini Bahati hatimaye amejibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na mchekeshaji Eddie Butita ambaye alidai kwamba bahati aliiba wazo lake na kulitumia kwenye kipindi cha mapishi ambacho kinaendeshwa na mkewe diana marua kwenye mtandao wa Youtube.

Akiwa kwenye moja ya Interview Bahati amesema hafahamu tuhuma za wizi wa haki miliki zilizoibuliwa na Butita ambapo ameenda mbali na kusema kwamba huenda mchekeshaji huyo anatumia jina lake kujitafutia umaarufu.

Hitmaker huyo wa “Pete Yangu” amekanusha kufanya mradi wowote na Butita ikizingatiwa kuwa hajawahi aanda mkutano wowote wa kibiashara na mchekeshaji.

Hata hivyo baada ya bahati kutoa upande wake wa stori, Butita alichukua video ya Bahati akikanusha madai hayo na kushare kwenye mitandao yake ya kijamii ambapo amedai kuwa yeye bado ni shabiki wa kazi wanaoifanya Bahati na mkewe.

Ikumbukwe wiki iliyopita Butita aliibuka na kudai kwamba kipindi cha “Cook na Reveal” chake Diana Marua ni wazo la kampuni yake ya “Stage Presence Media” na ilimchukua miezi mitatu kuja wa wazo la kipindic hicho.

 

Na baada ya kipind hicho kufanya vizuri msimu wa kwanza, Bahati alitafuta wadhamini wapya bila ya kumshirikisha, na mwisho wa siku akamkimbia

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke