You are currently viewing Bahati akerwa na kitendo cha mashabiki kumuita mheshimiwa

Bahati akerwa na kitendo cha mashabiki kumuita mheshimiwa

Msanii nyota nchini Bahati amewaonya mashabiki dhidi ya kumuita Mheshimiwa ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu ashindwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

Kupitia mitandao yake ya kijamii hitmaker huyo wa Adhiambo ameshangazwa na kitendo cha watu kumhusisha na jina hilo kila mara huku akiwataka kutumia jina la Bahati ambalo amekuwa akilitumia kwenye muziki

“Sielewi Mbona Bado Watu Wananiita MHESH… Niiteni tuu Bahati Please.” Ameandika Instagram.

Lakini pia Bahati amewataka mashabiki kuacha kumhusisha na siasa kwa sababu amerudi kwenye shughuli ya muziki ambayo amekuwa akifanya kwa muda mrefu.

“Hii Mambo Ya Mhesh Wekeni Kando…. THE KING IS BACK!!! Tell Me. What Happened While I Was Away???”, Ameongeza.

Bahati ambaye alikuwa kimya kwa miezi miwili baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Mambo ya Mhesh”

Utakumbuka Bahati alikuwa anawania kiti cha ubunge Mathare kupitia tiketi ya chama cha jubilee lakini alishindwa na mpenzani wake Anthony Oluoch wa chama cha ODM.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke