You are currently viewing BAHATI AKIRI BADO NI MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI

BAHATI AKIRI BADO NI MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI

Hitmaker wa ngoma ya “Adhiambo”, Msanii Bahati amedai kwamba bado yeye ni msanii wa injili kwani alimuahidi Mungu kwamba hatawahi kumuacha.

Akizungumza kwenye mahojiano na Mzazi Willy M. Tuva, msanii huyo amesema kwamba mafanikio yake katika maisha yameletwa na neema ya Mungu, hivyo basi hawezi kuziacha njia zake.

Katika hatua nyingine Bahati ametusanua kuhusu ndoto yake ya kuwa rais wa Kenya mwaka wa 2037 kwa kusema kwamba amekuwa akiota ndoto hiyo kwa kipindi kirefu tangu alipokalia kiti cha rais kwenye mkutano wa kisiasa huko Kasarani.

Utakumbuka Bahati alikuwa mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika juzi kati lakini kwa bahati mbaya alishindwa baada ya mpinzani wake Anthony Oluoch kuibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha ubunge eneo hilo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke