You are currently viewing BAHATI AKIRI  KUHONGWA MILLIONI 50 KUJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE MATHARE

BAHATI AKIRI KUHONGWA MILLIONI 50 KUJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA UBUNGE MATHARE

Staa wa muziki nchini  Bahati amefunguka tusioyajua kuhusu azma yake ya  kuwa mwanasiasa

Akizungumza na Radio Citizen, Bahati amesema alihongwa shilling millioni 50 kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Mathare ili kumpa nafasi mpinzani wake Anthony Oluoch nafasi ya kiti chake kwa mara ya pili kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Msanii huyo amesema kuwa wapinzani wake wote si wakazi wa Mathare na wamekuwa wakimshirikisha kwenye mazungumzo ili kumshawishi kulegeza msimamo wake wa kuwania ubunge wa eneo hilo.

“Niliambiwa nitapewa kazi. Lakini sitafuti kazi, najitafutia riziki kutokana na muziki wangu,” alisema.

Watu wamekuja na ofa wanataka kunilipa ili niondoke madarakani. Wamenipa mamilioni, hadi Ksh.50 milioni. Wanajua wakifika ofisini watapata pesa hizo,” Bahati alisema.

Kulingana na hitmaker huyo wa ngoma ‘Sweet Love’, ambaye anagombea ubunge kupitia tiketi ya chama cha Jubilee, washindani wake wamegundua kuwa hawezi kuhujumiwa kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa Mathare na sasa wanatumia njia zingine kumshawishi.

Bahati amemtaja mpinzani wake Anthony Oluoch, kuwa mmoja wa wale waliomwendea, wakiomba msaada wake.

“Aliniambia nimfanyie wimbo wa kampeni na kumuunga mkono. Wanataka kumtumia mtu kutoka Mathare kufika kwa watu,” aliongeza.

Hata hivyo ameapa kutojiondoa katika kinyang’anyiro cha ubunge Mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9 kwani hakuna marafiki wa kweli katika siasa.

“Ninakosa marafiki wa kweli, kwenye siasa unakaa na rafiki ambaye anasema asichomaanisha. Wanasiasa wengi si wa kweli,” alisema.

Matamshi ya Bahati yanajiri wakati ambapo yuko katika njia panda na Muungano wa Azimio la umoja, ambao hivi majuzi ulimtangaza Anthony Oluoch kama mgombeaji wao wanayempendelea kuwania kiti cha ubunge Mathare.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke