Nyota wa muziki nchini Bahati ameingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya magari ya Hava Cabs inayojihusisha na uchukuzi.
Bahati ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Hava Cabs.
Hitmaker huyo wa “Pete Yangu” sasa atatakiwa kutangaza huduma za Hava Cabs kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongeza kampuni hiyo wateja.
Bahati ni mmoja wa mastaa wa humu nchini ambao kati siku za hivi karibuni wamepata ubalozi wa makampuni mbali mbali kutokana na ushawishi wao mkubwa kwenye jamii.
Mpaka sasa mwanamuziki huyo amelamba dili ya ubalozi na kampuni ya Zunguka Africa safaris lakini pia ubalozi wa unga wa ugali wa Raha Premium