You are currently viewing BAHATI AMVUA NGUO EDWIN SIFUNA NA RACHAEL SHEBESH KISA SIASA ZA MATHARE

BAHATI AMVUA NGUO EDWIN SIFUNA NA RACHAEL SHEBESH KISA SIASA ZA MATHARE

Msanii aliyegeukia siasa nchini Bahati amemtolea uvivu katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna na Rachael Shebesh baada ya wawili hao kumtaka ajiuzulu kwenye azma yake ya kuwania ubunge ili kumpisha mbunge wa sasa wa Mathare Anthony oluoch kutetea kiti chake.

Msanii huyo amewasuta vikali wawili hao kwa kueneza propaganda kuwa amejiondoa kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare huku akiwataka wakome kuitaja jina lake kwenye siasa zao duni.

Bahati amesema hakuna kitu kitamzuia kwenye azma yake ya kuwawakilisha wakaazi wa Mathare bungeni baada ya uchaguzi wa Agosti 9 licha ya kupewa vitisho na kuzushiwa taarifa za uongo.

Kauli ya bahati imekuja mara baada ya mwenyekiti wa Jubilee kaunti ya Nairobi kudai kuwa Bahati atajiondioa kama mwaniaji wa ubunge mathare kumpisha mbunge wa sasa Athony Oluoch kutetea kiti chake kwani ni chaguo lao kama muungano wa Azimio.

Hii sio mara ya kwanza kwa azma ya Bahati kuwa mbunge wa Mathare kukumbwa na matatizo, mapema mwezi Aprili mwaka huu chama cha Jubilee ilitupilia mbali cheti chake kwa ajili ya kumshinikiza ampishe mbunge wa sasa Athony Olouch awe mwaniaji wa ubunge Mathare kupitia chama cha ODM.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke