Wakati ukichukulia poa siku ya Valentines, Staa wa muziki nchini Kenya Bahati hakuwa na jambo dogo kwa Baby Mama wake Diana B , kwani amempatia zawadi ya gari aina ya Land Cruiser Prado TX yenye thamani ya shillingi millioni 6.9.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diana B ametoa shukrani za dhati kwa mumewe Bahati kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea,ikizingatiwa kuwa Land Cruiser Prado TX ni gari ya ndoto yake.
“Sina neno, sina la kusema, Sipumui. Asante mpenzi Bahati. Tumetoka mbali na tunaweza kufika mbali zaidi kutoka hapa. Umetimiza ndoto zangu zote”.
“Gari hili ni zawadi yangu kwa bidii yangu katika kutengeneza content, bado nimeshtuka. Shukran. Sijui nilifanya nini ili nistahili wewe. Kila siku, namshukuru Mungu kwa ajili yako. Daima akupe neema kati ya wanaume wengine. Nakupenda Bahati” amesema.
Hii sio mara ya kwanza kwa Bahati kumnunulia mkewe wake Diana B zawadi za mkwanja mrefu kwani kipindi cha nyuma alimzawadi gari aina ya Mercedes Benz wakisherekea mitano ya ndoa lakini pia aliwahi kumnunulia shamba ya hekari mbili kama zawadi ya kumbukizi yake ya kuzaliwa