You are currently viewing BAHATI ANYANG’ANYWA CHETI CHA KUWANIA UBUNGE MATHARE

BAHATI ANYANG’ANYWA CHETI CHA KUWANIA UBUNGE MATHARE

Mwanamuziki aliyegeukia siasa Bahati amenyang’anywa tiketi ya kuwania ubunge wa Mathare kupitia chama cha Jubilee ikiwa ni siku chache zimepita tangu ashinde kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama hicho.

Katika mkao na wanahabari Bahati amesema alishurutishwa kujiuzulu kama mgombea wa kiti cha ubunge wa Mathare katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 mwaka huu baada ya muungano wa Azimio la Umoja kuamua kumuunga mkono mgombea wa ODM ambaye ni mbunge wa sasa Tom Oluoch.

Hata hivyo, amemtaka Kiongozi wa Chama cha Jubilee Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kuwapa wakazi wa Mathare nafasi ya kumchagua mbunge wao wanayempenda kwa kuwa alijiunga na siasa baada ya kupewa shinikizo na wapiga kura wa eneo hilo.

Utakumbukwa Mnamo Machi 18, Bahati alitangaza kuwa amejiunga na chama tawala cha jubilee na alikabidhiwa tikiti ya moja kwa moja na chama hicho kuwania kiti cha ubunge wa Mathare

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke