Staa wa muziki nchini Bahati ametunukiwa tuzo ya Golden Plaque na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers millioni moja kwenye channel yake.
Bahati ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi.
Channel ya youtube ya Bahati ilifunguliwa rasmi Joined Agosti 7, mwaka 2012 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 193,565,094 huku ikiwa na jumla ya subscribers 1,090, 000.
Bahati ni msanii wa pili nchini Kenya kupokea golden Plaque baada ya Otile Brown ambaye alikuw msanii wa kwanza nnchini kufikisha jumla y wafuatiliaji million moja YouTube.
Itakumbukwa tuzo ya Golden plaque imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ambao channel zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea.