You are currently viewing BAHATI ATANGAZA KUFANYA HOME COMING YAKE WIKIENDI HII HUKO MATHARE, NAIROBI

BAHATI ATANGAZA KUFANYA HOME COMING YAKE WIKIENDI HII HUKO MATHARE, NAIROBI

Nyota wa muziki nchini Bahati ametangaza kufanya ziara yake iitwayo ‘Bahati Mtoto wa Mama Home Coming’ Machi 27 mwaka huu katika uwanja wa Huruma grounds, Kaunti ya Nairobi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema amehamua kuja na ziara hiyo kwa ajili ya kunadi sera zake kwa wakaazi wa Mathare kama mbunge wao mtarajiwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Mbali na hayo, amesema kutakuwepo na fainali za soka katika uwanja wa Mathare Grounds ambapo timu ya Asec Huruma FC itachuana na Oostrom FC kwenye fainali huku Lucio FC ikicheza na True Colours FC kwenye mchezo wa kutafuta timu itakayochukua nafasi ya tatu.

Hata hivyo Bahati amesema timu ambayo itaibuka kidedea kwenye fainali hizo itatunukiwa shillingi elfu 150 huku nafasi ya pili na tatu ikizawadiwa shillingi elfu 100 na 50 mtawalia.

Utakumbuka Bahati anawania kiti cha ubunge eneo la Mathare kupitia tiketi ya chama cha Jubilee.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke