You are currently viewing BAHATI ATANGAZA KUWANIA UBUNGE MATHARE KWENYE UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9, 2022

BAHATI ATANGAZA KUWANIA UBUNGE MATHARE KWENYE UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9, 2022

Mwanamuziki nyota nchini Kevin Kioko, maarufu kama Bahati, ametangaza kuwania kiti cha ubunge wa eneo la Mathare katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022 kwa tiketi ya Chama cha Jubilee.

Akizungumza katika makao makuu ya Jubilee jijini Nairobi ambako alipokelewa na maafisa wa chama hicho Bahati amesema amechukua hatua ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kutokana na kero mbali mbali ambazo wakazi wa mathare wamekuwa wakikumbana nazo kwa muda mrefu.

“Changamoto yetu kubwa kama watu kutoka Mathare ni kwamba hatujawahi kumchagua kiongozi ambaye alizaliwa na kukulia Mathare. Tumekuwa tukichagua viongozi lakini wakati umefika kwa Mathare kupata mtoto wa kiume aliyezaliwa na kukulia huku Mathare ambaye ana elewa changamoto ambayo wananchi wanapitia,” mwanamuziki huyo amesema alipokuwa akiwahutubia wanahabari.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema iwapo atachaguliwa kama bunge wa mathare atahakikisha anatetea maslahi ya wananchi akiwa bungeni, kwani atakuwa mmoja ya watunga sheria na hivyo hatowaangusha.

“Tumekuwa tukilia mara kwa mara kwa sababu ya masuala yale yale na unajua ukitegemea mgeni akuongoze, hajui matatizo unayopitia,” Bahati amesema.

“Wakati umefika wa kubadilisha nyumba yangu, ni wakati wa kubadilisha historia yangu na ninakotoka…ndiyo maana ninawania kama Mbunge wa eneo bunge la Mathare kwa tiketi ya Jubilee,” mwimbaji huyo wa ngoma ya “Wa Nani” amesema.

Lakini pia ametangaza kuunga mkono azma ya kiongozi wa chama cha (ODM) Raila Odinga kuwania urais chini ya muungano wa Azimio la Umoja.

Bahati sasa atachuana na mbunge wa sasa wa mathare Anthony Oluoch ambaye alinyakua kiti hicho mwaka wa 2017 kwa tiketi ya chama cha ODM.

Utakumbuka juzi kati Bahati  aliachia wimbo uitwao  ‘Fire’ aliyomshirikisha Raila Odinga ambapo kwenye wimbo huo amemmiminia sifa nyingi kiongozi huyo wa Chama cha ODM akielezea mambo mengi ambayo ameifanyia nchi ya Kenya na kuahidi  kwamba iwapo Raila Odinga atachaguliwa kuwa rais Agosti 9, mwaka 2022 ataleta mabadiliko mengi nchini .

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke