You are currently viewing BAHATI ATANGAZA MSIMAMO WAKE KISIASA, AACHIA WIMBO UNAOMPIGIA DEBE RAILA ODINGA KWENYE AZMA YAKE YA URAIS.

BAHATI ATANGAZA MSIMAMO WAKE KISIASA, AACHIA WIMBO UNAOMPIGIA DEBE RAILA ODINGA KWENYE AZMA YAKE YA URAIS.

Staa wa muziki nchini Bahati amehamua kutangaza msimamo wake wa kisiasa ikiwa ni siku chache imepita tangu msanii mwenzake Willy Paul atangaze kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga.

Kupitia wimbo wake mpya uitwao Fire ambao amemshirika Raila Odinga bahati ameonekana kumwagia sifa kinara huyo wa chama odm jambo ambalo limetafsiriwa moja kwa moja kuwa amehamua kumuunga mkono odinga kwenye azma yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu kupitia muungano wa Azimio la umoja.

Hata hivyo wimbo huo wa Bahati umeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wameonekana kumpongeza kwa hatua ya kuweka msimamo wake kisiasa huku wengine wakimkosoa kwa hatua ya kuukimbia mrengo wa kenya kwanza ambao unaongozwa na naibu wa raias dakta William Ruto kupitia chama chake cha UDA.

Utakumbuka mwaka wa 2021 Bahati pia alitangaza kumuunga mkono naibu rais dakta William Ruto kwenye azma yake ya kuliongoza taifa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke