You are currently viewing BAHATI ATUHUMIWA KUIBA IDEA YA WIMBO WA JE UNANIFIKIRIA KUTOKA KWA MARIOO

BAHATI ATUHUMIWA KUIBA IDEA YA WIMBO WA JE UNANIFIKIRIA KUTOKA KWA MARIOO

Mkali wa muziki nchini Bahati ameingia tena katika mijadala kwenye mitandao nchini  baada ya kudaiwa kuiba  idea ya wimbo wa  ‘For You’ wa msanii  wa Bongofleva Marioo

Kulingana na ripoti inayosambaa mitandaoni, inadaiwa Bahati ametumia mdundo na ubunifu wa video wa wimbo huo kwenye wimbo wake mpya wa”Je unanifikiria”, hivyo kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao walienda mbali zaidi na kuhoji kuwa msanii huyo amekosa ubunifu kwenye muziki wake.

Hata hivyo Bahati hajetoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoibuliwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke