You are currently viewing BAHATI AWEKA WAZI GHARAMA YA KAMPEINI YAKE YA KISIASA

BAHATI AWEKA WAZI GHARAMA YA KAMPEINI YAKE YA KISIASA

Mwanamuziki Kevin Bahati Kioko maarufu kama Bahati ambaye pia ni mgombea Ubunge katika Jimbo la Mathare kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu nchini, amefunguka kiasi cha pesa ambacho ametumia hadi sasa kwenye kampeni zake.

Kwenye mahojiano yake na Millard Ayo, Bahati ambaye anagombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha Jubilee amesema ametumia kiasi cha shillingi millioni 33 za Kenya kuendesha kampeni zake.

Mbali na hilo Hitmaker huyo wa Adhiambo amesema ametenga zaidi ya KSh. 10 millioni kwa ajili ya siku ya Uchaguzi tu ambao utafanyika Kesho Jumanne huku akisisitiza kuwa pesa za kampeini zake za kisiasa zilitoka kwa wasamaria wema  wakiwemo marafiki pamoja na chama chake cha Jubilee.

Hata hivyo Bahati ambaye anawania kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu amedokeza kwamba ana mpango wa kuwania wadhfa wa juu kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2037, akisema ni ndoto yake kuwa rais wa taifa la Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke