You are currently viewing BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA RAILA ODINGA KUSHINDWA KUMTAMBUA JUKWAANI

BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA RAILA ODINGA KUSHINDWA KUMTAMBUA JUKWAANI

Staa wa muziki nchini Bahati amezua gumzo mtandaoni mara baada ya mgombea wa urais kupitia Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga kushindwa kumtambua akiwa jukwaani.

Raila ambaye alikuwa anawatambulisha wagombea wa viti mbali mbali vya kisiasa kupitia Azimio la Umoja huko Kamkunji, jijini Nairobi alijipata amemuita Bahati jina la Mathew baada ya wandani wake kujaribu kumtambulisha msanii huyo kwake.

Sasa jambo hilo limezuia mjadala mzito miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi wameonekana kumkejeli Bahati wakihoji ni kwa nini Raila alishindwa kumtambua msanii huyo mbele ya umma ikizingatiwa Bahti mwenyewe amekuwa akijinadi kwamba ana ukaribu na mgombea huyo wa urais kupitia muungano wa Azimio laUmoja.

Hata hivyo wafuasi wa Raila Odinga wameonekana kumkingia kifua mwanasiasa huyo kwa kusema kwamba ana mambo mengi ya kuwaza kutokana na shinikizo za uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita Bahati aliachia wimbo wa uitwao “Fire” aliyomshirikisha Raila Odinga ambapo alimwagia sifa kinara huyo wa chama cha ODM kwenye azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke