Staa wa muziki nchini Bahati amefuta picha na video zake kwenye mtandao wa Instagram, hatua iliyohisiwa ni ujio wake mpya.
Hatua hii ya Bahati imevuta hisia za baadhi ya mashabiki ikihisiwa kuwa huenda akaachia kazi mpya hivi karibuni baada ya kukaa kimya tangu apoteze kiti cha ubunge mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika nchini kenya.
Uamuzi wa Bahati hakujali hata picha alizopiga na mke wake, Diana B huku upande mwingine ikihisiwa kuwa pengine kuna kingine kisichohusiana na ujio wa kazi kutoka kwake.
Utakumbuka juzi kati Bahati alifunguka kuwa familia yake ipo njia panda ambapo aliwataka mashabiki kumweka kwenye maombi pamoja na mke wake Diana ambaye alikuwa mbioni kujifungua.