Wanandoa mashuhuri nchini Diana Marua na Bahati wamefichua kuwa wanatarajia kupata mtoto wa tatu hivi karibuni.
Wakitoa taarifa hiyo njema kwenye chaneli yao ya You Tube, wanandoa hao wamesema kwamba tayari ‘wanampenda’ mtoto wao huyo ambaye hajazaliwa.
“kila siku nakutafutia , kwa vile nakulombotov … nakutamkia baraka, nakutakia fanaka, kutoa sadaka nyota yako itawaka, tamka isiyokua na mipaka … malaika wakulinde … na si twakusiburi kama mwisho …” wamesikika wakiimba kwenye video waliyoichapisha chaneli zao za Youtube.
Wawili hao wana watoto wawili pamoja, Heaven na Majesty na mashabiki wamewapongeza kwa mafanikio hayo huku wakiwatakia heri wakati huu wanatarajia kumpata mtoto wao wa tatu.