You are currently viewing BAHATI NA DIANA MARUA WATANGAZWA MABALOZI WA OPPO KENYA

BAHATI NA DIANA MARUA WATANGAZWA MABALOZI WA OPPO KENYA

Kampuni ya OPPO inayojishughulisha na  uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki imemtangaza rasmi  Bahati na mke wake Diana Marua kuwa mabalozi wake.

Katika taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa instagram katika page ya Oppo Kenya imeeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha Bahati pamoja na Diana Marua kuwa balozi wa Oppo.

“We partnered with @wabosha_maxine @bahatikenya @diana_marua to officially introduce you all to our newest model, the OPPO Reno 7!”,  Imesema sehemu ya chapicho hilo.

Kwa upande mwingine Bahati amethibitisha pia katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram kwa kusema kwamba amejisikia faraja kuwa balozi  wa OPPO na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu.

“ANNOUNCEMENT‼️ JUST SIGNED AS THE NEW OPPO Reno 7 BRAND AMBASSADORS 🔥 So excited to partner with @oppo_kenya @wabosha.maxine and Wifey @Diana_Marua as we officially introduce to you the new OPPO Reno 7!”,  imesema taarifa hiyo.

Wakati huo huo Oppo imeitambulisha simu yake mpya ya Oppo Reno ambayo imeingia hivi karibuni sokoni, simu hiyo yenye 8GB RAM + 250 GB ROM inatarajiwa kuuzwa kwa bei nafuu zaidi ili kumsaidia kila Mkenya kumiliki smartphone.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke