You are currently viewing BAHATII AIDHINISHA NA TUME YA IEBC KUWANIA UBUNGE MATHARE AGOSTI 9

BAHATII AIDHINISHA NA TUME YA IEBC KUWANIA UBUNGE MATHARE AGOSTI 9

Msanii aliyegeukia siasa Kevin Kioko Bahati  amethibitisha rasmi na tume ya IEBC kuwa miongoni mwa wagombea watakaowania ubunge Mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Hii ni baada ya tume hiyo kuorodhesha jina lake kwenye gazeti lake rasmi licha ya Muungano wa Azimio la Umoja kumtaka ajiondoe kwenye kinyanganyiro cha ubunge mathare kwa ajili ya kumpa nafasi mbunge wa sasa Anthony Oluoch kutetea kiti chake.

Kulingana na notisi hiyo Bahati atawania ubunge Mathare kupitia tiketi ya chama ya jubilee.

Bahati amepokea taarifa hiyo kwa furaha huku akisema kuwa IEBC imeheshimu matakwa ya wakaazi wa eneo bunge la Mathare.

“When Jesus says yes, nobody can say no! I have been the most fought MP candidate; my loosing opponent tried everything to threaten me & make sure I step down but look at what God has done! It’s official now,”  Ameandika kupitia  twitter.

Bahati kwa sasa atachuana na wagombea wengine wa ubunge mathare kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke