You are currently viewing BARNABA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

BARNABA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki Barnaba ameachia rasmi Album yake mpya “Love Sounds Different” yenye Jumla ya mikwaju 18 yenye uzito wa miaka (18) ambayo amekuwepo kwenye huu muziki.

Album hiyo imesheheni majina mazito yanayotamba kwenye Muziki wa bongo fleva, Kolabo za nguvu zimesogezwa na Diamond Platnumz, AliKiba, Marioo, Kusah, Dayoo, Jux, Lunya, Mbosso, Saraphina, Khadija Kopa, Lady Jaydee, Jay Melody, Lody Music, Nandy, Rayvanny, Platform na wengine akiwemo pia Khaligraph Jones toka Kenya.

Jina la Diamond Platnumz mbali na kutokea kwenye wimbo namba 1 “Hadithi” lakini limetajwa kama Mtayarishaji Mkuu wa Album hiyo (Executive Producer) wakiwemo pia watayarishaji wengine kama Abbah Process, S2Kizzy, Man Walter, Chizan Brain, Mr. Simon, Laizer Classic na wengine

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke