Mwanamuziki nyota kutoka nchini Tanzania Barnaba Classic ametimiza ndoto nyingine kubwa katika hatua za kukamilisha Album yake ijayo ambayo amewashirikisha wakali kibao.
Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kutimiza ndoto yake ya kufanya kazi na Malkia wa taarab Bi. Khadija Kopa huku akithibitsha kuwa atakuwa miongoni mwa walioshirikishwa kwenye Album yake ijayo.
Hata hivyo Barnaba ameongeza kuwa album yake ijayo itaacha kumbukumbu kwenye muziki wa Tanzania.