You are currently viewing BARNABA CLASSIC MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

BARNABA CLASSIC MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki nyota  wa Bongo Fleva, Barnaba Classic amesema kuwa album yake ijayo itakuwa Bora kwa mwaka 2022.

Barnaba ametoa sifa hiyo juu ya album yake kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram, huku akieleza kuwa ameshirikiana na wasanii wengi wa ndani na nje ya Tanzania.

“Kwanza muziki nilioutumia” ameeleza Barnaba ikiwa hiyo ni sababu ya kwanza. “Nimetoa nafasi kwa new generation (vizazi vipya) kunipa mchango wa mawazo”. Sababu ya tatu Barnaba ameeleza, “Ndio album yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushirikisha wenzangu wengi, ndani na nje ya nchi”.

Aidha, barnaba classic amedai album yake imekamilika kwa aslimia 78% na atatoa mwongozi ikishakuwa tayari.

Album hiyo inaenda kuwa album ya tano kwa mtu mzima barnaba classic tangu aanze kufanya  muziki wa bongofleva miaka 20 iliyopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke