Staa wa muziki wa Bongofleva Barnaba Classic yupo mbioni kuufungua ukurasa mwingine wa mapenzi kwa tukio la kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi bibie Raya The Boss ikiwa ni kiashiria cha kuelekea katika ndoa.
Barnaba amebainisha ujio wa jambo hilo la kheri kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare picha ya pete mbili na kuwapa nafasi mashabiki wake wamchagulie ipi itafaa kumvisha mpenzi wake huyo.
“Ipi itafaa, she says Yes ” – ameandika Barnaba.
Uhusiano wa wawili hao ulianza mwaka 2018 baada ya Barnaba kuachana na aliyekuwa mpenzi wake.