Baada ya msanii wa Comedy nchini Eric Omondi kudai kuwa Amapiano imeuwa muziki wa Bongo Fleva,wasanii wa Tanzania Zuchu na Barnaba Classic wameibuka na kupinga hilo.
Wasanii hao wamesema kwamba wanachokifanya kwa sasa ni kutaka kukimbizana na nyakati zilizopo kwani kuwa kwenye kiwanda cha muziki ambacho kina ushindani kunahitaji msaani kuwa na ubunifu
Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Bongo Fleva bado ina nguvu sana kuliko Amapiano. Watu wajue Amapiano sio aina ya muziki bali kwa lugha rahisi ni mixing za Dj’s wa Arika Kusini so haitoweza kuuwa Bongo Fleva”
Kwa upande wa Zuchu ameandika kuwa “Bongo Fleva haitotokea kufa wasanii wanabadilika hii inaitwa mabadiliko, kujaribu ladha mpya hakujawahi kuuwa soko la muziki. Acha wasanii wajaribu vitu vipya ndio mabadiliko hayo”