You are currently viewing BASATA YASITISHA UTEUZI WA STEVE NYERERE KUWA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

BASATA YASITISHA UTEUZI WA STEVE NYERERE KUWA MSEMAJI WA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA

Baraza la Sanaa la Tanzania – BASATA limemtaka Msemaji wa Shirikisho la Muziki nchini humo, Steve Nyerere asianze kutekeleza majukumu yake hadi pale mamlaka hiyo itakapofahamu kiini cha mgogoro wa uteuzi wake na kupata ufumbuzi kwa mujibu wa katiba na sheria.

BASATA imesema inafanyia kazi taarifa zilizowasilishwa na shirikisho pamoja na hoja za wajumbe waliohudhuria kikao kilichofanyika machi 21 mwaka huu kuhusu uteuzi wa nafasi hiyo, ambapo katika kikao hicho wadau wa muziki tanzania walisema Steven Nyerere hawezi kuwa msemaji wala mhamasishaji wa muziki..

Hata hivyo Muda mfupi baada ys Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kumtaka Steve Nyerere kutoanza kazi kama Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania, msanii huyo ameshukuru kwa kusema kwamba anaheshimu uamuzi huo.

“Niseme asante Basata, asante sana haki inabaki pale pale, pole jirani na tupo pamoja yaliyopita si ndwele tugange yajayo”

“Basata imesema kwamba sasa inafanyia kazi taarifa ya shirikisho na hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao.” ameandika Steve Nyerere Instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke