Mwanamuziki Moses Ssali maarufu Bebe Cool ni mmoja wa wasanii waliokosolewa zaidi nchini Uganda, lakini huenda wanaomchafulia jina wakijipata hatiani hivi karibuni.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na MwanaYouTube wa eneo hilo, bosi huyo wa Gagamel ameeleza kuwa ameanza kukusanya ushahidi dhidi ya wanahabari ambao wamekuwa wakimpaka tope kwa tuhuma za uongo.
“Nimejenga brand yangu kwa muda mrefu sana na kwa mwandishi yeyote wa habari kuja kuniongelea upuuzi, nawaahidi nitawapa funzo. Ninakusanya ushahidi, na watalipa,” alisema.
Hata hivyo Bebe Cool amesema washukiwa wakuu ni watangazaji wa redio na TV ambao wamekuwa wakitoa maoni hasi dhidi yake.