You are currently viewing BEBE COOL AAHAPA KUIKINGIA KIFUA FAMILIA YA BOBI WINE

BEBE COOL AAHAPA KUIKINGIA KIFUA FAMILIA YA BOBI WINE

Mwanamuziki Bebe Cool hana mahusiano mazuri na msanii mwenzake Bobi Wine, lakini katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Bebe Cool amehibitisha kwamba hawezi kumvumilia mtu yeyote atakayeitupia matusi familia ya Bobi Wine hasa mkewe na watoto wake.

Hitmaker huyo wa “Wire Wire” amesema licha ya kwamba yeye na Bob wine sio marafiki wa karibu, ataikingia kifua familia yake kwa udhalilishaji wowote kutoka kwa mashabiki zake.

Bosi huyo wa Gagamel ameenda mbali zaidi na kusema kwamba bifu lake na Bobi wine ni wa kiitalaam na wala sio wa kibinafsi kama namna wengi wanavyodhani.

Bebe Cool na Bobi Wine wamekuwa na ugomvi kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda kwa takriban miongo miwili.

Mara ya mwisho wawili hao kukutana uso kwa uso ilikuwa mwaka mwaka wa 2018 katika Hoteli ya Serena jijini Kampala kwenye tamasha la muziki la msanii Eddy Kenzo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke