You are currently viewing Bebe Cool achoshwa na wasanii wa Nigeria kutumbuiza nchini Uganda

Bebe Cool achoshwa na wasanii wa Nigeria kutumbuiza nchini Uganda

Msanii mkongwe nchini Uganda Bebe Cool amechoshwa na hatua ya wasaniii wa Nigeria kutumbuiza nchini humo kila wiki.

Bebe cool amesema kitendo hicho imewafanya wasaniii wa Nigeria kujiona kuwa wana mashabiki wengi kuwashinda wasanii wa ndani huku akiwataka mashabiki kuwaonyesha upendo wasanii wa Uganda pindi wanapofanya matamasha kama njia ya kuwapa changamoto mapromota muziki kuwazingatia kwenye maonyesha yao.

“We are tired of Nigerian artists coming here and acting as though they have more fans here. I implore everyone who has supported Kenzo to also come for Jose Chameleone’s concert dubbed “Gwanga Mujje” next year at Cricket Oval,” Alisema Bebe Cool.

Bosi huyo wa Gagamel ametoa kauli hiyo alipokuwa anawarai mashabiki kumuunga mkono msanii jose chameolene kipindi hiki yupo kwenye maandalizi ya onesho lake ambalo litafanyika mapema mwaka 2023.

Ikumbukwe ndani ya mwaka huu wasanii kumi kutoka Nigeria tayari wametumbuiza nchini Uganda akiwemo Tiwa Savage, Rema, Ruger, na wengine wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke