Mwanamuziki kutoka Uganda Bebe Cool amefunguka na kudai kwamba hana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni kwani ana miaka 20 ya kufanya hivyo.
Kwenye moja ya onesho lake huko Kawempe Bebe Cool amesema ndio mwanzo anaanza safari yake ya muziki hivyo mashabiki watarajie muziki mzuri kutoka kwake.
“Majuzi niliambia Chameleone kuwa nina mpango wa kustaafu muziki miaka 20 ijayo na akaanza kuachia muziki maana alikuwa amelaza damu.”..Amesema Bebe Cool
Bebe Cool ambaye ana umri wa miaka 40 ametoa changamoto kwa wasanii wachanga kutia bidii kwenye kazi zao maana wasanii wakongwe hawana mpango wa kuacha muziki.
Utakumbuka Bebe Cool ni mmoja kati ya wasanii wakongwe kwenye muziki nchini Uganda kwani amekuwa kwenye game ya muziki kwa takriban miongo miwili.