You are currently viewing BEBE COOL AFUNGUKA MPANGO WA KUMALIZA BIFU YAKE NA BOBI WINE

BEBE COOL AFUNGUKA MPANGO WA KUMALIZA BIFU YAKE NA BOBI WINE

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amefunguka kuhusu suala la kumaliza ugomvi wake na msanii aliyegeukia siasa nchini humo Bobi Wine.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool ameweka wazi matamanio yake ya kuzika tofauti zake na Bobi Wine kwa manufaa ya tasnia ya muziki ya nchini uganda wakiwemo mashabiki na wananchi kwa ujumla.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Genyvudde” amesema kwamba hatua hiyo itasaidia kuleta amani kwa kupunguza chuki miongoni mwa wafuasi wao.

Licha ya kuweka wazi mpango wake huo Bebe Cool amesema hilo litafanyika tu iwapo Bobi Wine atamuomba baba yake msamaha kwa kuvunjia heshima kipindi cha nyuma.

Utakumbuka Bebe Cool na Bobi Wine kipindi cha nyuma walikuwa marafiki wakubwa kwenye muziki wao lakini walikuja wakakosana na kila mmoja akaenda kivyake kama msanii wa kujitegemea na tangu wakati huo wamekuwa wakishindana kisiasa, kimuziki na hata kifedha.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke