Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amedai kwamba hana mpango wa kustaafu muziki licha ya kuwa kwenye game kwa takriban miongo miwili.
Akizungumza kwenye moja ya interview Hitmaker huyo wa “Boss Lady” ambaye juzi kati alikuwa anasherekea miaka 45 tangu kuzaliwa kwake, amesema hatostaafu muziki katika kipindi cha miaka 5 ijayo kama alivyosema awali, ila ataendelea kufanya kazi hiyo hadi kifo chake.
Hata hivyo Staa huyo amesisitiza kuwa kiwanda cha muziki nchini Uganda bado kinamuhitaji ikizingatiwa kuwa bado hajafanikisha ndoto yake ya kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa.
Utakumbuka mwanamuziki Bebe Cool aliwahi kusema kuwa atastaafu mara tu atakapofikisha umri wa miaka 50, lakini kutokana na kauli yake hii inaoneka ataendelea kuwabariki mashabiki zake na muziki mzuri licha ya walimwengu kuhoji kwamba anatumia ushirikina kuwavuta mashabiki.