Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Bebe Cool amefunguka kuhusu ugonjwa uliompelekea kukimbizwa hospitali mwishoni mwa juma lilopita.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Bebe Cool ameweka wazi kuwa alikuwa anaugua malari, ugonjwa ambao hakuwa fikiria utampata.
Hitmaker huyo “Gyenvudde” amesema kwa sasa amepata ufahamu wa kwanini Wizara Afya nchini Uganda imekuwa mstari wa mbele kusisitiza umuhimu wa kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Tamko la Bebe Cool limekuja mara baada ya tetesi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa msanii alikimbizwa hospitali baada ya kukutwa na kirusi cha Omicron