You are currently viewing BEBE COOL AKANUSHA TUHUMA ZA KUMNYANYASA MSANII CHIPUKIZI

BEBE COOL AKANUSHA TUHUMA ZA KUMNYANYASA MSANII CHIPUKIZI

Mwezi mmoja uliopita, msanii nguli nchini uganda Bebe Cool aliachia wimbo uitwao “Gyenvudde” ambao unasimulia maisha yake kwenye muziki. Wimbo huo ambao bado haujapata mapokezi mazuri unadaiwa kwamba uliandikwa na msanii chipukizi kwa jina la black Skin.

Juzi kati msanii huyo aliibuka na kudai kwamba Bebe Cool alishindwa kumlipa licha ya kumuandikia wimbo wa Gyenvudde”. Black Skin alisema baada ya Bebe Cool kushindwa kumlipa pesa zake alihamua kurekodi na kuachia wimbo wa Gyenvudde”  kama njia ya kuonyesha kutoridhishwa na kitendo cha bosi huyo wa Gagamel.

Sasa Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Bebe Cool amedai kwamba Black Skin anatumia jina lake kujitafutia umaarufu kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda kwani ameshindwa na suala la kuachia muziki mzuri.

Kulingana na Bebe Cool, alilipa gharama zote za kutayarisha wimbo wake wa Gyenvudde”, hivyo alishtuka baada ya black skin kuibua madai  hayo.

Ikumbukwe black skin anatajwa kuhusika kwenye uandishi wa wimbo wa Bebe Cool uitwao ‘Katono’.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke