Msanii mkongwe kwenye muziki Bebe Cool ameamua kumpa maua yake Eddy Kenzo akiwa angali hai licha ya watu kuhisi kuwa ana bifu (ugomvi) na Bosi huyo wa Big Talent.
Mkali huyo ngoma ya “Boss Lady” ametoa wito kwa mashabiki wa muziki mzuri kujitokeza na kuhudhuria tamasha la msanii huyo Novemba 12 huko Kololo Airstrip huku akithibitisha kuwa atakuwa moja kati ya wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo.
Ikumbukwe miaka kadhaa iliyopita Eddy Kenzo alimualika Bebe Cool kwenye tamasha lake la muziki katika hoteli ya Serena viungani mwa Jiji la Kampala na kupitia tamasha hilo ndipo alimaliza bifu yake na Bobi Wine.