You are currently viewing BEBE COOL AMVUA NGUO DIAMOND PLATINUMZ, ADAI ANAISHA MAISHA YA KUIGIZA

BEBE COOL AMVUA NGUO DIAMOND PLATINUMZ, ADAI ANAISHA MAISHA YA KUIGIZA

Msanii nguli nchini Bebe Cool amezilaumu vyombo vya habari nchini uganda kwa kuzitangaza sana nyimbo za msanii wa bongofleva Diamond Platinumz kuliko nyimbo za wasanii wa nchini hiyo.

Akiwa kwenye moja ya Interview Bebe Cool amesema watangazaji wa redio na runinga wamewaaminisha mashabiki wa muziki nchini uganda kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko msanii yeyote Afrika mashariki jambo ambalo amedai kwamba sio kweli.

Bosi huyo wa Gagamel ameenda mbali zaidi na kusema kwamba Diamond Platinumz hana cha kujivunia kwenye maisha yake kwani anaishi maisha ya kuigiza ili tu abaki kwenye midomo ya wapenzi wa muziki mzuri afrika mashariki.

Hata hivyo Bebe Cool amejinasibu kwa kusema kwamba yeye, Bobi Wine na Jose Chameleone walinunua magari ya kifahari kama Escalade na Hummer wakiwa na umri mdogo hivyo Diamond Platinumz hana jipya la kuwaonyesha

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke